TETESI ZA SOKA KATIKA MAGAZETI YA ULAYA ...! ZIKO HAPA MTU WANGU
Barcelona wanajiandaa kutibua mpango wa Manchester United, kwa kumnyakua
kiungo kutoka Colombia, Juan Cuadrado, 26, kutoka Fiorentina (Daily
express), Paris Saint-Germain wamekubaliana kimsingi na Real Madrid
kumsajili Angel Di Maria (Sport), hata hivyo Man U wanadaiwa kutoa dau
la pauni milioni 55 sawa na PSG ili kumshawishi winga huyo (Metro),
mashambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo, 29, amesema katika soka
chochote kinaweza kutokea na huenda kuna uwezekano wa kurejea Old
Trafford (Manchester Evening News), meneja wa Manchester City Manuel
Pellegrini ameambiwa beki wa Porto Eliaquim Mangala, 23, atakuwa
mchezaji wa mwisho kusajiliwa msimu huu (Times), Barcelona na Brondby ya
Denmark wanafikiria kumchukua beki wa kati wa Liverpool Daniel Agger,
29, kufuatia kuwasili kwa beki Dejan Lovren kutoka Southampton (Daily
Mail), Arsenal wapo tayari kumsajili beki wa zamani wa Liverpool Alvaro
Arbeloa, 31, kutoka Real Madrid, iwapo Thomas Vermaelen, 28, ataondoka
Emirates (AS), Manchester United wapo tayari kumsajili Vermaelen kwa
pauni milioni 12, licha ya kuwa beki huyo ni majeruhi baada ya kuumia
wakati wa Kombe la Dunia akiwa na Ubelgiji (Guardian), Liverpool
wamepata kikwazo katika jaribio lao la kumsajili mshambuliaji Ezequiel
Lavezzi kutoka PSG, baada ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Argentina
kutaka kwenda Juventus (Daily Express), boss wa Newcastle Alan Pardew
amesema amekata tamaa kumfuatilia Loic Remy, 27, kutoka QPR (Newcastle
Chronicle), West Ham wanajiandaa kutaka kumsajili mshambuliaji wa Stoke
City Peter Crouch, 33, kuimarisha safu ya ushambuliaji baada ya Samuel
Eto'o kushindwa kuafikiana na Upton Park (Daily Star), kipa wa
Southampton Artur Boruc, 34, ananyatiwa na Bayern Munich (Telegraph),
Liverpool 'watawasaidia' Manchester United katika mchakato wao wa
kumsajili Mats Hummels, 25, kwa kumruhusu beki wao Tiago IIori, 21,
kwenda Borussia Drotmund kwa mkopo (Daily Star), Everton na Norwich
wanataka kumsajili mshambuliaji kutoka Gambia Modou Barrow, 21,
anayechezea Ostersunds FK (Sky Sports), Tottenham wanafanya mazungumzo
na beki kutoka Argentina, Mateo Musacchio, 23, anayechezea Villareal.
Mchezaji huyo alihusishwa na kwenda Barcelona pia (Daily Mirror), QPR
wanafikiria kumchukua kiungo Mauricio Isla, 26, kutoka Juventus kwa
mkopo (Daily Mail), mshambuliaji wa Tottenham Emmanuel Adebayor, 30,
ataanza mazoezi siku ya Jumamosi lakini anasema alijisikia dhaifu sana
baada ya kupata malaria mwezi Juni hakuweza hata kutembea (Sun), kocha
wa Real Madrid, na meneja wa zamani wa Chelsea, Carlo Ancelotti amesema
itakuwa "vigumu" kwa Louis van Gaal kuibadili Manchester United na kuwa
timu inayowania ubingwa msimu huu (Guardian), kiungo wa England Ashley
Young, 29, yuko tayari kucheza kama 'beki-winga' ili kufufua matumaini
yake chini ya meneja mpya Van Gaal (Daily Mirror), meneja wa Arsenal,
Arsene Wenger ametabiri kuwa ushindani utakuwa mkali sana msimu huu
kutokana na sheria mpya za usawa wa kifedha ambazo zitawaathiri mahasimu
wa Arsenal (Times) kipa wa zamani wa Chelsea Mark Bosnich anaamini Petr
Cech, 32, ataondoka Darajani msimu huu, iwapo atakuwa namba mbili nyuma
ya Thibaut Courtois, 22, (Talksport), mshambuliaji wa Arsenal Theo
Walcott, 25, ametoa onyo kwa mahasimu wa Arsenal, kupitia twitter
akisema "wamwangalie sana" Alexis Sanchez akisema atakuwa hatari. Tetesi Na salim kikeke- Cheers!
No comments