Breaking News

AJALI....!! BASI LA AM COACH LAPINDUKA WILAYANI MASWA NA KUJERUHI

Basi la AM Coach likiwa eneo la tukio katika kijiji cha Sayusayu wilayani Maswa mkoani Simiyu

Habari za hivi punde  zilizoufikia  ni kwamba Basi la AM COACH lililokuwa linatoka Meatu mkoani Simiyu  kwenda Mwanza limepinduka katika kijiji cha Sayusayu wilayani Maswa mkoani Simiyu.

Kwa mujibu wa habari kutoka eneo la tukio watu sita wamejeruhiwa na wamekimbizwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwani hali za ni mbaya.

Miongoni mwa waliojeruhiwa yumo mtoto mwenye umri wa miaka mitano.
Chanzo Malunde1 blog

No comments