Breaking News

JEZI ZA JAMES RODRIGUEZ ZAWEKA REKODI REAL MADRID

Screen Shot 2014-07-24 at 9.33.54 AMMuda mfupi baada ya kujiunga na Real Madrid kwa ada ya uhamisho wa paundi millioni 63, mchezaji wa Colombia James Rodriguez ameweka rekodi katika mauzo ya jezi yake ya Real Madrid.
Ripoti za Hispania zinasema Jezi zipatazo 50000 za James Rodriguez zimeuzwa ndani ya siku  moja tangu zilipoingia rasmi sokoni ambapo zimeuzwa kwenye duka la Real Madrid na imeonyesha kiasi gani raia huyu wa Colombia anavyokubalika.

Rodriguez ametua Madrid akitokea AS Monaco huku akiwa ndiye mfungaji bora wa Kombe la Dunia nchini Brazil 2014 baada ya kutokana na magoli 6 aliyofunga.

No comments