UKRAINE WASEMA INAOUSHAHIDI URUSI KUFYATUA KOMBORA LILILOANGUSHA NDEGE YA MALYSIA
Ukraine imesema inao ushahidi thabiti kuonyesha kwamba waliokuwa wanausimamia mfumo wa makombora uliotumika katika kuiangusha ndege ya abiria ya Malayasia ni raia wa Urusi na kwamba lazima wahojiwe.
Hayo ameyasema Mkuu wa Ukraine wa kupambana na ujasusi Vitaly Nada.
Nada ameeleza kwenye mkutano na waandishi wa habari mjini Kiev kuwa Ukraine inao ushahidi thabiti kwamba kitendo cha kigaidi cha kuiangusha ndege ya Malaysia kilifanyika kutokana na msaada wa Urusi. Amesema Ukraine inafahamu fika kwamba mfumo wa makombora ulikuwa unadhibitiwa na raia wa Urusi.
Wakati huo huo kiongozi wa waasi wa mashariki mwa Ukraine Alexander Borodai amesema visanduku vya kunakilia safari za ndege ya Malaysia ilioanguka ndani ya Ukraine havijaonekana.
No comments