FIFA YALEGEZA ADHABU KWA SUAREZ
FIFA imesema Luis Suarez ataruhusiwa kufanya mazoezi na Liverpool wakati akitumikia adhabu yake ya miezi minne na mechi nane za kimataifa.
Wakati huohuo Uruguay imekata rufaa kupinga adhabu hiyo.
Suarez alifungiwa
"shughuli zote zinazohusu kandanda" baada ya kumng'ata Georgio Chiellini wa Italy.
Hata hivyo Claudio Sulser, mkuu wa kamati ya nidhamu ya FIFA alipoulizwa siku ya Alhamisi mjini Rio de Janeiro kuhusu adhabu hiyo alisema:
Sulser pia amethibitisha kuwa Uruguay imekata rufaa kupinga adhabu iliyotolewa.
Claudio Sulser pia amesema Suarez ambaye anasakwa na Barcelona, ataruhusiwa kuhusika katika mchakato wa uhamisho.
No comments