Breaking News

"TUMEKAMATA WASHUKIWA WA MAUAJI " ISRAELI YASEMA

Taarifa kutoka nchini Israeli zinasema kuwa serikali inawazuia baadhi ya watu kwa 
tuhuma za kuhusika na mauaji ya kijana wa kipalestina Mohammed Abu Khdeir.
Mauaji hayo kwa mjibu wa polisi nchini humo yanahusishwa na hamasa za utofauti wa utaifa .

Israel imeyatuhumu makundi ya kijeshi ya wapiganaji wa Kipalestina wa Hamas kwa mauaji hayo.Hata hivyo mauaji hayo yamechukuliwa kama ni ulipizaji kisasi dhidi ya mauajia ya wanaharakati wa kiyahudi kutokana na kuuawa kwa vijana watatu mwezi uliopita.
Kundi la Hamas wao wamekanusha kuhusishwa na mauaji hayo.
Idara za usalama za Israeli zinamshikilia raia wa Palestina anayedaiwa kuhamasihsa mauaji hayo ya vijana wa Israel.

No comments