Chelsea yaichapa Burnley 3-1
Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho
Chelsea ilipeleka kilio kwa Burnley usiku wa jumatatu katika mchuano wa ligi kuu ya England ambapo Chelsea iliitandika Burnley mabao 3-1.
Burnley ilitangulia kufunga bao moja dhidi ya Chelsea kupitia mchezaji wake Scott Arfield katika kipindi cha kwanza cha mchezo hali iliyotishia kuwa pengine Chelsea ingepoteza katika mchezo huo, hata hivyo , goli hilo halikudumu kwa muda mrefu,ambapo kazi nzuri ya wachezaji wa Chelsea kama vile Diego Costa,Ivanovich na Andre Shule ilitosha kabisa kuitoa jasho Barnley.
No comments