NORA AKANA KUCHOROPOA MIMBA

Msanii aliyewahi kutamba miaka ya nyuma na kundi la Kaole Nuru Nassoro 'Nora' ameamua kufunguka baada ya tuhuma nzito iliyokuwa inamkabili ya kudaiwa kuchoropoa mimba ya msanii mwenzake.....
Nora anadaiwa kuwa katika uhusiano na mmoja wa wasanii wa siku nyingi huku wiki za hivi karibuni akifululiza kwenda hospitali na wambeya wakadai ni ujauzito na kwamba yupo kwenye harakati za kuutoa...
Nora mwenyewe akiongea na mwandishi wa habari hii aliweka wazi kuwa suala la kwenda hospitali kupima ni kawaida yake na kwamba maneno hayo yanakuzwa na wabaya wake....
"Hakuna suala kama hilo. Hivi mtu kwenda kucheki afya yako ndo kutoa mimba? mbona wapo wanaokesha huko na hawasemwi? Sina mpango huo na huyo msanii anayejitapa kuwa nimetoa mimba yake nikimjua atanieleza ni lini nililala naye mpaka akanipa mimba",alisema Nora
No comments