Breaking News

KORTINI KWA KUPIGA SELFIE ABU DHABI

Robert BlackHii inatufundisha na sisi tunaopenda kuchukua selfie au kupiga picha kwenye mazingira mazuri tunapofika kwenye nchi za watu, kuna maeneo mengine unaweza kupiga picha kwa nia nzuri alafu ukajikuta kwenye matatizo kama ya Robert Alan Black.
Robert ambae ni raia wa Marekani alikamatwa huko Abu Dhabi falme za kiarabu October 21 baada ya kupiga picha kwenye eneo ambalo hairuhusiwi mtu yeyote kuinyanyua camera yake.
Kwa kipindi chote mzee huyu mwenye umri wa miaka 70 alikua akishikiliwa huku kesi yake ikiwa Mahakamani ambapo serikali yake ya nchi yake iliingilia kati na hatimaye Mahakama ikatangaza kumwachia huru baadae baada ya kugundulika kwamba hakukusudia kupiga picha kwa makusudi na sasa yuko huru.

Abu DhabiUnaambiwa ni watu wengi hukamatwa na kushikiliwa kwa kisa kama hiki huko Abu Dhabi na mara nyingine ni kweli wanapiga picha kwenye maeneo yasiyoruhusiwa ambapo wengi wanaohojiwa baada ya kukamatwa wanasema hawakuona vibao vinavyokataza wao kupiga picha, vibao vipo ila huwa inatokea bahati mbaya tu hawajaviona.

No comments