VIDEO: P-SQUARE WAACHIA KICHUPA KIPYA BAADA YA EJEAJO WALIOMSHIRIKISHA T.I
Sherehe ya kuazimisha mwaka mmoja wa ndoa ya Peter Okoye ambayo ilikuwa jana Novemba 17 siku ambayo wamesherehekea pia siku yao ya kuzaliwa, mastaa hao wasiochuja kwenye muziki kutoka Nigeria P Square wameitumia siku hiyo pia kusherehekea na fans wao duniani kwa kuachia Video ya wimbo wao mpya unaoitwaShekini.
P Square wameachia video hiyo inayopatikana katika albam ya sita waliyoiachia hivi karibuni ya “Double Trouble”, ni imani yangu unajua uzuri wa kazi za mastaa hao, unadhani hii itaweza kuendelea kuwaweka kwenye level za juu kwenye muziki?
Producer wa Video ni Clarence Peters aliyewahi kufanya kazi na mastaa kama Davido, Iyanya, na Yemi Alade na akashinda tuzo nyingi ikiwemo kubwa ya mtayarishaji bora wa Video Afrika ya MTV Africa Music Awards 2014.
Najua una hamu ya kuiona video hiyo, nimekuwekea hapa mtu wangu unaweza kuitazama hapa na nitafurahi kuona comment yako.
No comments